1 / 14

Huduma baada ya kujifungua

Huduma baada ya kujifungua. Taarifa anayotakiwa kupewa kijana baada ya kujifungua:. Kujadiliana kuhusu wasiwasi na matatizo aliyonayo. Kufuatiliwa matatizo aliyokuwa nayo wakati wa ujauzito kama kukataliwa na aliyempa mimba, alikuwa haipendi/haitaki mimba. Upungufu wa damu.

jayme
Télécharger la présentation

Huduma baada ya kujifungua

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. Huduma baada ya kujifungua

  2. Taarifa anayotakiwa kupewa kijana baada ya kujifungua: • Kujadiliana kuhusu wasiwasi na matatizo aliyonayo. • Kufuatiliwa matatizo aliyokuwa nayo wakati wa ujauzito kama kukataliwa na aliyempa mimba, alikuwa haipendi/haitaki mimba. • Upungufu wa damu. • Kuzungumzia uzazi wa mpango na umuhimu wa kujikinga na magonjwa ya ngono.

  3. Taarifa …. • Muda wa kupumzika na mazoezi. • Lishe bora ili kurudisha afya yake na kwa maziwa ya mtoto. • Kuhudhuria kliniki ili kuangaliwa afya yake na mtoto • Usafi wa mama na mtoto • Upendo kwa mtoto • Umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama

  4. Ahsante kwa kunisikiliza

  5. Huduma baada ya mimba kuharibika

  6. Maana ya kuharibika kwa mimba • Ni kuharibika/kukatishwa kwa mimba katika umri wa chini ya miezi 7 (wiki 28). Mimba inaweza kutoka yenyewe au kutolewa makusudi.

  7. Aina za kuharibika kwa mimba • Kutoka yenyewe Ni mimba zinazoharibika na kutoka bila kuchokonolewa/kuchokozwa. Hii huweza kusababishwa na homa kama za malaria, magonjwa ya ngono, matumizi ya madawa makali au kupigwa.

  8. Mimba iliyotolewa • Ni kutoka kwa mimba baada ya kuchokonolewa/kuchokozwa kama kwa kumeza madawa kwa makusudi hayo, kuingiza vijiti au vyombo kwenye shingo ya mji wa mimba. Pia mimba huweza kutolewa kama kuna sababu na ushauri wa daktari (inapotishia uhai)

  9. Dalili za mimba inayotoka • Maumivu ya tumbo chini ya kitovu • Mtoto kuacha kucheza • Mwili kuishiwa nguvu • Damu kutoka ukeni • Majimaji yenye harufu kutoka ukeni • Kichefu chefu na hata kutapika

  10. Madhara ya kutoa mimba • Maambukizi • Kupoteza damu nyingi • Kuumizwa via vya uzazi • Kuathirika na sumu ya dawa zilizotumika kutoa mimba • Kuwa tasa/ugumba • Kifo

  11. Jinsi ya kuzuia utoaji mimba • Kuacha ngono • Kutumia kinga kwa usahihi kama njia za uzazi wa mpango • Kutumia njia ya uzazi wa mpango za dharura

  12. UMUHIMU WA HUDUMA KWA KIJANA ALIYEHARIBU MIMBA (POST ABORTION CARE) • Huduma ni muhimu kwa kijana balehe ili kuzuia madhara yatokanayo na kuharibu mimba.

  13. Taarifa anayotakiwa kupewa kijana aliyeharibu mimba: • Huduma hii inapatikana katika vituo vya afya. • Inatolewa na mtoa huduma mwenye utaalamu huo • Ni haki ya kijana • Mimba nyingine inaweza kutunga siku saba baada ya kuharibika

  14. Taarifa anayotakiwa kupewa kijana aliyeharibu mimba: • Njia za uzazi wa mpango isipokuwa kitanzi, zinaweza kutumiwa mara baada ya mimba kuharibika. • Epuka kufanya ngono hadi damu baada ya kuharibika mimba itakapokoma, kwa kufanya hivyo kuna hatari ya kupata maambukizo.

More Related