1 / 19

Neno la Uzima

Neno la Uzima. Desemba 2012. Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu (Yh 1:12). Tazama, habari kuu mpya iliyotangazwa na Yesu, na kuwapatia wanadamu tunu: kuwa wana wa Mungu, kufanyika kuwa wana wa Mungu kwa njia ya neema.

dori
Télécharger la présentation

Neno la Uzima

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. Neno la Uzima Desemba 2012

  2. Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu (Yh 1:12)

  3. Tazama, habari kuu mpya iliyotangazwa na Yesu, na kuwapatia wanadamu tunu: kuwa wana wa Mungu, kufanyika kuwa wana wa Mungu kwa njia ya neema.

  4. Lakini jinsi gani na kwa nani hutolewa neema hiyo? “Kwa wote waliompokea” na wote watakaompokea katika karne zijazo.

  5. Lazima kumpokea katika imani na katika upendo, kwa kusadiki kwa Yesu kama Mkombozi wetu

  6. Lakini tujitahidi kufahamu kwa kina zaidi maana yake nini kuwa watoto wa Mungu.

  7. Inatosha kumtazama Yesu, Mwana wa Mungu, na uhusiano wake na Baba: Yesu alikuwa akimwomba Baba yake kama alivyofanya katika sala ya “Baba yetu”. Kwake yeye, Baba alikuwa “Abbà”, yaani neno analotamka mtoto kwa baba yake mzazi peke yake, akamwelekea na maneno ya kumtegemea yasiyo na kifani, na upendo usio na mipaka.

  8. Lakini, kwa sababu alikuja duniani kwa ajili yetu, hakuridhika kuwa yeye tu katika hali hii ya pekee.

  9. Kwa kufa kwa ajili yetu, kwa kutukomboa, ametufanya kuwa watoto wa Mungu, dada na kaka zake, na akatupatia nasi, kwa njia ya Roho Mtakatifu, uwezo wa kuingia ndani kabisa ya Utatu Mtakatifu.

  10. Hivyo nasi pia tunajaliwa kutumia tamko hilo: Abbà, Baba (Mk 14:36; Rm 8:15): “Baba, babangu”, Baba yetu, pamoja na yote yafuatayo nayo: hakika ya ulinzi wake, usalama, kujiaminisha kwa upendo wake, matulizo ya Mungu, nguvu, moto; moto unaozaliwa moyoni kwa yule aliye na hakika ya kupendwa.

  11. Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu (Yh 1:12)

  12. Kile kinachotufanya kitu kimoja na Kristo na wana ndani yake ni Ubatizo, na maisha ya neema yanayotokana nao..

  13. Katika mstari huo wa Injili kuna, pia, neno linalodhihirisha uhai wa kina wa “Umwana” huo wa kutekeleza siku kwa siku. Naam, lazima “kufanyika watoto wa Mungu”.

  14. Kufanyika, kukua kama wana wa Mungu, kwa kuitika kipaji chake, kuishi mapenzi yake yaliyomo yote katika amri ya upendo: kwa Mungu na kwa majirani.

  15. Yaani, kumpokea Yesu, maana yake ni kumpokea katika majirani yetu wote. Nao pia wataweza kuwa na uwezo wa kumtambua Yesu na kumwamini, ikiwa katika moyo wetu watatambua alama, cheche ya mwanga wa upendo usio na mipaka ya Baba.

  16. Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu (Yh 1:12)

  17. Katika mwezi huu, tunapokumbuka hasa Kuzaliwa kwake Yesu duniani hapa, tujitahidi kumpokea kila mmoja wenzake, kwa kumwona na kumtumikia Kristo mwenyewe kila mmoja kwa wenzake.

  18. Basi, mabadilishano wa upendo, wa kuyajua maisha kama yale yanayounganisha Mwana kwa Baba katika Roho Mtakatifu, yatasimika pia kati yetu na Baba, na tutahisi kufikia daima katika ulimi wetu tamko la Yesu: «Abbà, Baba!»

  19. Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu (Yh 1:12) “Parola di Vita” inatangazwa na Movement of Focolare. Matini hii Imetolewa katika Città Nuova, 1998/22, p. 37Chapa cha Anna Lollo akishirikiana na Fr. Placido D’Omina (Sicily, Italy). Maelezo ya Neno la Uzima inatafsiriwa katika lugha 96 na kilugha na kuwafikia mamilioni ya watu katika dunia nzima kwa njia ya maandishi, radio, TV na kwa njia ya Tovuti. Kwa kupata maelezo www.focolare.org PPS hiyo, katika lugha mbalimbali inatangazwa katika www.santuariosancalogero.it (na hapo unaweza kupakua)

More Related