1 / 27

MDAHALAO WA UWEZESHAJI KIUCHUMI WA MKOA WA MWANZA

MDAHALAO WA UWEZESHAJI KIUCHUMI WA MKOA WA MWANZA. Uliofanyika Mwanza Juni 10, 2008. Utangulizi. Mwanza una wilaya nane -Geita -Sengerema -Kwimba -Ukerewe -Misungwi -Magu -Nyamagana -Ilemela. Utangulizi. Eneo la kilometa za mraba 35,187 Kilometa za mraba 15,092 (43%) ni maji

jamar
Télécharger la présentation

MDAHALAO WA UWEZESHAJI KIUCHUMI WA MKOA WA MWANZA

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. MDAHALAO WA UWEZESHAJI KIUCHUMI WA MKOA WA MWANZA Uliofanyika Mwanza Juni 10, 2008

  2. Utangulizi • Mwanza una wilaya nane -Geita -Sengerema -Kwimba -Ukerewe -Misungwi -Magu -Nyamagana -Ilemela

  3. Utangulizi • Eneo la kilometa za mraba 35,187 • Kilometa za mraba 15,092 (43%) ni maji • Shughuli kubwa za kiuchumi ni -Kilimo -Ufugaji -Uvuvi -Uchimbaji madini • Idadi ya watu ni milioni 3.5

  4. Hali ya Uchumi na Umaskini • Pato la mkoa ni sh. milioni 961,672 (nafasi ya 2 kitaifa) • Pato la mkoa la kila mtu ni sh. 309,577 (nafasi ya 12 kitaifa) • Kiwango cha umaskini ni 48.33% (nafasi ya 18 kitaifa)

  5. Matokeo Kutokana na Ripoti za Wilaya • Maeneo 9 ya kupewa kipaumbele katika uwezeshaji wa kiuchumi katika mkoa wa Mwanza. -Kilimo -Uvuvi -Ufugaji -Biashara na viwanda

  6. Matokeo Kutokana na Ripoti za Wilaya -Madini -Utalii -Nishati -Misitu -Taasisi za fedha na mitaji

  7. Kilimo • Fursa -Hali ya hewa nzuri • Matatizo -Uhaba wa ardhi -Utegemezi kwa mvua, -Tija ndogo kwenye kilimo -Bei ndogo ya mazao

  8. Kilimo Mikakati • Wilaya zipangiwe mazao mawili ya kulima kutokana na ubora wa mazingira yake badala ya kila wilaya kulima mazao yote • Kuboresha na kuanzisha vituo vya mafunzo ya kilimo na kuwa na mashamba darasa ili kuongeza tija • Kuanzishwa kwa kilimo cha alizeti

  9. Kilimo • Kuanzisha maghala ya kijiji • Kushawishi serikali kuu iwekeze kwenye maghala ya kisasa ya wilaya • Kuanzisha kilimo cha majaluba karibu na ziwa Viktoria • Kuboresha uelimishaji wa wakulima wadogo ili kuboresha tija kwenye kilimo • Kuwezesha watu wachache wenye uwezo ili wafanye ukulima wa kisasa

  10. Uvuvi • Fursa -Nguvukazi ya uvuvi • Vikwazo -Uvuvi usio endelevu -Usalama majini

  11. Uvuvi Mikakati • Kuboresha taarifa za masoko na bei ya samaki. • Kuhamasisha uanzishwaji wa mabwawa ya kufuga sato ili kufanya uvuvi uwe endelevu. • Kuboresha usimamizi wa serikali kwenye sekta ya uvuvi ili wavuvi wasionewe kibei.

  12. Uvuvi • Kuanzisha minada ya samaki ili iwe sehemu pekee ya kuuza na kununua samaki ili kusaidia wavuvi kupata bei nzuri. • Ujenzi wa mabwawa ya kuzuia maji ili kuwezesha ufugaji samaki. • Kuongeza bidii kudhibiti uvuvi haramu

  13. Ufugaji • Fursa -Uwepo wa mifugo mingi • Kikwazo -Ubora duni wa mifugo kitija

  14. Ufugaji Mikakati • Kuboresha aina ya ng’ombe kwa kufanya “breeding” ili kupata ng’ombe wakubwa zaidi wenye kutoa ngozi, nyama na maziwa zaidi. • Kuelimisha wakulima juu ya faida ya kubadilisha aina ya ng’ombe.

  15. Ufugaji • Serikali kuu isaidie kuboresha kituo cha Mabuki. • Kuanzishwa kwa ufugaji wa mbuni na mamba kwa ajili ya kuuza bidhaa zake kibiashara. • Ufugaji wa wanyamapori katika zoo ili kuvutia watalii

  16. Biashara na Viwanda • Fursa -Nguvukazi • Kikwazo -Upatikanaji mgumu wa mikopo

  17. Biashara na Viwanda Mikakati • Serikali itoe guarantee ya mikopo ya wafanyabiashara wadogo na wa kati. • Kuhamasisha serikali kupunguza idadi ya wadhibiti ili kupunguza gharama za kufanya biashara. • Kuhamasisha wafanyabiashara kuongeza thamani kwenye bidhaa wanazonunua kabla ya kuuza.

  18. Biashara na Viwanda • Kuwajengea wamachinga mijini sehemu moja ya kufanyia biashara. • Kuhamasisha serikali kuu, kuhamasisha wawekezaji kuwekeza Mwanza kwa kuwapunguzia gharama za kufanya biashara. • Kuhamasisha serikali kabadili mfumo wa sheria ili kuiachia sekta binafsi kufanya shughuli zake ili kuinyanyua sekta binafsi

  19. Madini • Fursa -Wingi wa madini • Kikwazo -Mitaji midogo ya wachimbaji wadogo.

  20. Madini Mkakati • Kuwawezesha wachimabaji wadogo wawezeshwe kwa njia ya soko, vifaa na utafiti wawezeshwe kwa kupitia SACCOs.

  21. Misitu • Fursa -Hali ya hewa inayoruhusu kuota kwa miti ya aina mbalimbali • Kikwazo -Kupungua kwa miti

  22. Misitu Mikakati • Kuelimisha watu juu ya faida za kufuga nyuki wa asali kwa njia ya vikundi. • Kupanda miti kama mitiki na misandale kwa ajili ya kuuza nje na kuwezesha upatikanaji wa mkaa.

  23. Utalii • Fursa -Kuwepo sehemu za kitalii Mwanza na ukaribu wa mkoa na sehemu za kitalii • Kikwazo • Kutokufahamika sehemu za kitalii vizuri

  24. Utalii Mikakati • Kuhamasisha watalii wanaokwenda Serengeti kupitia Mwanza. • Kuhamasisha watu binafsi wawekeze kwenye marestaurant. • Kuandika nakala kuhusu historia ya mkoa na kuitawanya ili kuboresha ufahamu wa watu wa sehemu za kihistoria za mkoa. • Kuandika ripoti ya fursa za kitalii za mkoa wa Mwanza.

  25. Nishati • Kikwazo ni uhaba wa nishati umeme Mikakati • Kuvutia wawekezaji wa nishati ya umeme Mwanza. • Kuhamasisha utumiaji umeme wa jua, umeme wa wanyama kazi na dizeli vijijini.

  26. Taasisi za Fedha na Mitaji • Kikwazo ni ugumu wa taasisi za kifedha kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo kutokana na kutokuwa na imani nao

  27. Taasisi za Fedha na Mitaji Mikakati • Kuhamasisha uanzishwaji wa SACCOs • Uboreshaji wa SACCOs • Kuwapa mafunzo wafanyabiashara wadogo ili kuzifanya taasisi za kifedha ziwe na imani nao. • Kuanzisha benki ya wananchi ambayo wanahisa wakubwa ni SACCOs.

More Related