350 likes | 1.02k Vues
Hatua za makuzi kwa vijana. Hatua za makuzi na maendeleo kwa vijana. Umri wa kati ya miaka (10-13) Umri wa Kati ya miaka (14-16) Kijana wa rika kubwa miaka (17-19) . Mabadiliko yanayotokea kwa wasichana. Mwili kukua, kupanuka kwa nyonga, kukua kwa kwa matiti
E N D
Hatua za makuzi na maendeleo kwa vijana • Umri wa kati ya miaka (10-13) • Umri wa Kati ya miaka (14-16) • Kijana wa rika kubwa miaka (17-19)
Mabadiliko yanayotokea kwa wasichana • Mwili kukua, kupanuka kwa nyonga, kukua kwa kwa matiti • Ngozi kuwa nyororo, chunusi usoni • Kukua kwa via vya uzazi • Kuvuja ungo • Kuongezeka kwa hamu ya mahusiano ya kijinsia • Kupenda kuonekana nadhifu
Mabadiliko kwa wavulana • Kuongezeka urefu, uzito, kukua kwa misuli • Sauti kuwa nzito • Kuota chunusi usoni • Kuota nywele sehemu za siri • Kupata hamu ya kujamiiana
Mabadiliko ya kiakili katika umri tofauti kwa wasichana na wavulana Umri wa miaka 10 – 13 • Tabia ya kujaribu mambo • Uwezo wa kuchanganua mambo • Kupenda marafiki nje ya familia • Kupenda uamua mambo mwenyewe • Kupenda kusikiliza mawazo wa wanarika
Umri wa miaka 14 - 16 • Kupenda kuuliza dhamira za mitazamo na sera mbali mbali • Kukua kwa uwezo wa kufikiri matokeo ya tabia hatarishi • Kuongezeka zaidi kwa msukumo wa makundi rika • Kuongezeka kwa hamu ya kujamiiana na kupenda marafiki wa jinsi tofauti
Umri wa kati ya miaka 17 - 19 • Kupevuka kwa via vya uzazi • Kukua kwa uwezo wa kutatua matatizo • Kukua kwa uwezo wa kujitambua • Kupungua kwa msukumo wa makundi rika • Kushirikiana na familia/ kutoa mawazo yake • Kutopenda kukaa katika magurupu • Kukua kwa uwezo wa kushika majukumu ya familia • Anaelekea katika maisha ya kujitegemea
Vigezo vinavyohamasisha tabia ya kijana • Majukumu ya kijinsia • Msukumo wa makundi rika • Mahusiano na wazazi au watu wazima • Tabia ya kujiamini
Lengo: • Kuelezea nini maana ya mawasiliano • Vipengele wakati wa kufanya mawasiliano • Nini vikwazo vya mawasiliano
Maana ya mawasiliano • Ni mtiririko wa ujumbe kutoka kwa anayetuma kwenda kwa anayepokea.
Aina za mawasiliano • Mawasiliano ya mtu binafsi • Mawasiliano ya uso kwa uso baina na mtu na mtu au mtu na kikundi cha watu • Mawasiliano kwa kutumia vyombo vya habari
Mbinu za mawasiliano • Kusikiliza kwa makini • Kufafanua • Kuuliza maswali ya wazi (yanayomwezesha mtu kujieleza) • Kurudia kilichosemwa na mwingine kwa maneno yako bila kubadilisha
Mbinu za mawasiliano • Kutumia vihamasisho k.m. kutikisa kichwa, kutabasamu, kusema “aha!!” • Kutambua ishara zinazojitokeza wakati wa mawasilinao k.m. kukunja uso, na kuzifanyia kazi. • Kutoa muhtasari
Vipengele vya mawasiliano: • Mtuma ujumbe • Ujumbe • Njia ya kupitishia ujumbe • Mpokea ujumbe • Mrejesho
Sifa za mawasiliano ya uhakika • Mtoa ujumbe lazima awe na elimu ya kutosha • Awe anaipenda mada ya ujumbe • Awe anawajua walengwa • Awe anazungumza katika kiwango cha walengwa wake • Achague njia sahihi ya kutuma mawasiliano
Kazi ya vikundi Elezea ni vipi vikwazo vya mawasiliano?
Vikwazo vya mawasiliano • Umri • Jinsia • Mawazo • Kelele • Lugha • Mazingira • Mtazamo
Nini maana ya ushawishi wa afya ya uzazi kwa vijana • Ni kazi ya utoaji habari, elimu na ushauri kwa viongozi, wazazi na jamii kwa jumla ili waelewe, washawishike na kuunga mkono programu, shughuli au mawazo ya programu maalum.
Umuhimu wa kuendesha ushawishi: • Kujenga mwamko wa uelewa • Kubadili tabia/mwenedo • Kuungwa mkono • Kuhamasisha • Kutoa motisha • Kusaidia jamii kuchukua hatua za utekelezaji
Kanuni za kuendesha ushawishi:Ili ushawishi ufanikiwe mada inatakiwa: • Iende na wakati • Iwe thabiti • Iwe rahisi kueleweka • Ilingane na mahitaji ya afya ya vijana • Itoe ujumbe • Isibadilike badilike • Inayovutia
Namna ya kuendesha ushawishi • Wasalimie wahusika katika lugha inayokubalika • Eleza hali halisi ya afya ya uzazi na vijana katika jamii yao (Kijiji chao n.k.) • Eleza faida ya mikakati ya afya ya uzazi kwa vijana • Omba kuungwa mkono katika shughuli za afya ya uzazi kwa vijana • Funga mada/semina